Home Michezo VIBE LA SIMBA NA YANGA LAHAMIA ZANZIBAR…MAMILIONI YATENGWA KWA AJILI YAO…

VIBE LA SIMBA NA YANGA LAHAMIA ZANZIBAR…MAMILIONI YATENGWA KWA AJILI YAO…

Habari za Simba na Yanga

Watani wa jadi Simba, Yanga huenda zikahamishia uhasimu wao wa jadi katika soka la Tanzania Bara katika visiwa vya Zanzibar baada ya kupokea mualiko wa kushiriki kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup yatakayofanyika mwakani.

Timu zingine ambazo zimepokea mualiko ni Azam FC na Singida Big Stars katika mashindano ambayo yanatarajia kutimua vumbi kuanza Januari Mosi 2022.

Endapo timu hizo zitathibitisha ushiriki Singida BS kwa mara ya kwanza itaungana na mabingwa watetezi Simba, Yanga, Azam FC na Namungo kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye mashindano hayo.

Singida itakuwa ni msimu wake wa kwanza kwenye ushiriki wa mashindano hayo kwa upande wa timu za Tanzania Bara huku Azam FC ndiye kinara wa kutwaa mataji ya mashindano hayo akichukua mara tano.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano hayo, Khamis Abdalla Said anasema ni timu za Zanzibar pekee hadi sasa ambazo zimethibitisha ushiriki wa mashindani hayo.

“Timu za Zanzibar pekee ndio zilizothibitisha ushiriki hizo nyingine tumezipa mualiko wa mashindano hayo zikikubali kushiriki ndipo ratiba ya mashindano itatolewa,” anasema.

Anasema mashindano hayo yanatarajia kushirikisha timu 12 kutoka Tanzania Bara, Burundi na Zanzibar ambazo tayari wamezitumia mialiko ya ushiriki.

Mbali na wawakilizi wa Bara timu nyingine zitakazoshiriki katika michuano hiyo ni KVZ, KMKM, Mlandege, Jamhuri pamoja na timu ya Chipukizi zote kutoka Zanzibar na Aigle Noir kutoka Burundi.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA 'PASSWORD' ZA YANGA KUWA KMC...BUMBULI ASHINDWA KUVUMILIA..ALIPUKA HAYA...