Home Simba SC SIMBA SC WAZINDUA JEZI MPYA MAALUMU KWA AJILI YA AZAM TU.

SIMBA SC WAZINDUA JEZI MPYA MAALUMU KWA AJILI YA AZAM TU.


WEKUNDU wa Msimbazi Simba wameendelea kuonyesha jeuri ya pesa bwana baada ya leo kutambulisha rasmi jezi zitakazotumika kwenye Kombe la Shirikisho la Azam.

Juni 26 Simba watamenyana na Azam FC katika mchezo wa nusu fainali wa FA ambao utalindima katika Dimba la Majimaji Songea.

Simba ndiye bingwa mtetezi katika michuano hiyo hivyo itatumia uzi huo mpya.

Kupitia akaunti ya Instagram ya Simba leo imeziweka wazi jezi hizo aina mbili nyekundu na nyeupe ambazo zitatumika katika michezo miwili endapo watatinga fainali.


Jezi hiyo imeonekana kuwa gumzo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ya WhatsApp wengine wakiisifia na wengine wakiibeza pia.

Hivyo basi Simba msimu huu itakuwa inetumia jezi tatu tofauti ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa pamoja na FA ambayo imetambulishwa leo.

Tayari jezi hizo kwa mujibu wa msemaji wa Wekundu hao zinapatikana Tanzania nzima.

SOMA NA HII  SIMBA KUTAMBULISHA UZI MPYA LEO