Home Uncategorized SENEGAL YAKIRI MUZIKI WA UGANDA ULIKUWA WA MOTO

SENEGAL YAKIRI MUZIKI WA UGANDA ULIKUWA WA MOTO


LICHA ya kikosi cha timu ya Taifa ya Senegal kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Afcon nchini Misri, kocha wa Senegal, Aliou Cisse amesema kuwa alikutana na timu ngumu.

Bao pekee la ushindi la Senegal lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa anayekipiga Liverpool, Sadio Mane dakika ya 15 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo licha ya safu ya Uganda iliyo chini ya Emmmanuel Okwi kufanya majaribio mengi ambayo hayakuzaa matunda.

“Tumeshinda ila tulicheza na timu ngumu hali iliyotufanya tutumie mbinu ya kupaki basi kulinda ushindi wetu, wapinzani wetu walikuwa wanakuja sana kwenye eneo letu la hatari kutafuta matokeo, ila mwisho wa siku tunaanza kujipanga kwa hatua inayofuata ambayo ni robo fainali,” amesema Cisse.

Kocha wa Uganda,Sebastien Desabre amesema kuwa anapenda kuwapongeza wapinzani wake Senegal kwa kupata matokeo kwani walicheza na mchezaji ambaye yupo hatua nyingine kimataifa ila bado anajivunia wachezaji wake.

“Mane ni mchezaji wa Dunia hivyo ni ngumu kumzuia mchezaji kama yule ila mwisho wa siku tumepambanampaka hapa tulipofika,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA WAINYOOSHA MABAO 2-0 DAR CITY