Home Uncategorized KAGERA SUGAR: MSIMU UJAO TUTATISHA

KAGERA SUGAR: MSIMU UJAO TUTATISHA

KOCHA wa kikosi cha Kagera Sugar, Meky Maxime amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kufanya usajili makini utakaowafanya walete ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.

Msimu wa 2018-19 Kagera Sugar ilinusurika kushuka daraja jambo lililowapa darasa la kutosha na kuwafanya wajipange sawa sawa msimu ujao.

“Kwa sasa tumejipanga na tumeanza kazi ya kufanya usajili makini ambao utatufanya tulete ushindani msimu ujao, mpaka sasa kila kitu kipo sawa nina imani tutafanya makuwa msimu ujao.” amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamesajiliwa ndani ya Kagera Sugar ni pamoja na Evarigitius Mujwahuki kutoka Mbao FC na Hassan Isihaka kutoka Mtibwa Sugar.

SOMA NA HII  SIMBA YAINGIA ANGA ZA UD SONGO, KULIVUTA JEMBE HILI LA KAZI