Home CAF VIJANA WA IBENGE WAINGIA DOSARI…SAFARI YAO YAKWAMA…LIGI YA MABINGWA AFRIKA

VIJANA WA IBENGE WAINGIA DOSARI…SAFARI YAO YAKWAMA…LIGI YA MABINGWA AFRIKA

VIJANA WA IBENGE WAINGIA DOSARI...SAFARI YAO YAKWAMA...LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Miamba ya Soka kutoka nchini Misri, Timu ya Al Ahly wamefanikiwa kupenya hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa Al Hilal ya Sudan mabao 3-0.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na Timu zote kuwa na nafasi ya kusonga hatua ya Robo Fainali, iliwachukua Ahly dakika 25 tu kupata bao la kuongoza lililofungwa na Straika wake Mahmoud Kahraba kabla ya H. E. Shahat kupachika mabao mawili kipindi cha pili.

Kwa ushindi huo wa Ahly msimamo wa kundi B unabaki hivi;
Mamelodi Alama 14
Ahly Alama 10
Al Hilal. Alama 10
Cotton Sports Alama 0
Ahly wana magoli mengi ya kufunga tofauti na Hilal hivyo safari ya vijana wa Ibenge imekwamia hatua ya Makundi.

SOMA NA HII  YANGA WAFUNGUKA YA MOYONI...BADO TUNA KISASI NA RIVERS...WANEFICHUA HAYA