Home Uncategorized BEKI WA NKANA FC, HASSAN KESSY ATAJA ATAKAPOKUWA IWAPO DILI LAKE LITABUMA...

BEKI WA NKANA FC, HASSAN KESSY ATAJA ATAKAPOKUWA IWAPO DILI LAKE LITABUMA NKANA


HASSAN Kessy, beki wa Nkana FC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Zambia amesema kuwa akikwama kubaki ndani ya klabu hiyo ataibukia Afrika Kusini.

Mkataba wa Kessy ndani ya Nkana FC unameguka mwishoni mwa msimu huu na mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote na mabosi wake kutokana na shughuli za michezo kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.


Nyota huyo amesema kuwa hesabu zake ni kusonga mbele zaidi ya hapo alipo kwa sasa na anafikiria kwenda Afrika Kusini. 


“Nawaza kwenda kucheza mbele sio kurudi nyuma kwani kwa sasa mkataba wangu na Nkana unakaribia kuisha na hakuna mazungumzo ya kuongeza mkataba kwa kuwa michezo kule haijulikani itarejea lini,” .

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA HUU HAPA