Home Ligi Kuu MAISHA YANAKWENDA KASI, MAPAMBANO LAZIMA YAENDELEE

MAISHA YANAKWENDA KASI, MAPAMBANO LAZIMA YAENDELEE


 MAISHA yanakwenda kasi sana ambapo kwa sasa tayari Mwadui FC imeshaanza kupiga hesabu za kushiriki Ligi Daraja la Kwanza huku timu tatu nyingine zikiwa kwenye joto ya kutafuta hatma zao ndani ya ligi.

Hii yote inatokana na namna ambavyo timu hizo zilianza kujipanga mwanzo wa msimu na ikapata kile ambacho ilipanda.

Ukweli ni kwamba hakuna timu ambayo haina uwezo wa kutwaa kombe lolote katika mashindano na hakuna timu yenye uhakika wa kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara bado ni mipango na hesabu ambazo zinahitajika.

Hakuna namna nyingine ambayo inaweza kufanyika kwa sasa katika lala salama zaidi ya kila timu kushinda mechi zake na mwisho wa siku itajua kitu gani imevuna.

Ninachotaka kusema ni kwamba kwenye maisha ya soka iwe ni kuanzia Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili na Ligi ya Wanawake pia kinachohitajika ni maandalizi mazuri.

Ikiwa hakutakuwa na mwanzo mzuri basi mwisho nao utakuwa ni wa kuungaunga ambao matokeo yake huwa ni anguko kwa timu husika.

Tabia nyingine ambayo imekuwa ikizimaliza timu zetu Tanzania ni pamoja na mtindo wa kutimua makocha pamoja na kuanza maisha mapya na wachezaji wengi jambo ambalo limekuwa ni tatizo.

Ukiitazama Mwadui FC ambayo msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza ina ongezeko la wachezaji zaidi ya 10 katika kikosi cha kwanza wote wakiwa ni wapya na wameikuta timu ikiwa katikati ya ligi.

Haya ambayo yanatokea kwao sasa inamaanisha kwamba hawakujipanga na walipokuja kushtuka tayari mambo yamekuwa mazito kwao na wakawa hawana chaguo.

Sio Mwadui pekee hata Yanga nao wana ingizo kubwa la nyota wapya ambao wamewafanya na imekuwa ikiwapa tabu katika kupata matokeo.

Angalau kidogo kwa Yanga wengi walianza mzunguko wa kwanza pamoja ila bado waliongeza wengine dirisha dogo na kati ya hao ni wachezaji wawili wameingia moja kwa moja kikosi cha kwanza.


Hapa kuna jambo la kufanyia kazi kwa timu zetu ili kuweza kufikia mafanikio kwa sababu mafanikio ya mpira wetu yanahitaji maandalizi mazuri na ushindani kwa kila timu.

SOMA NA HII  HITIMANA: KAZI BADO INAENDELEA


Ukitazama kwenye hatua ya kimataifa angalau kidogo kuna mwanga umeanza kuonekana kwa kuwa wawakilishi wa msimu huu walijitahidi kupambania bendera ya Tanzania.


Namungo katika Kombe la Shirikisho wao walitinga hatua ya makundi ila ngoma ikawa nzito kwao katika mechi zote ambazo walicheza walishindwa kuvuna angalau pointi moja wala bao moja zote walipoteza.


Kwa upande wao naona kwenye mashindano hayo pia wametolewa hatua ya robo fainali katika Kombe la Shirikisho, hivyo hawana nafasi ya kuwakilisha Tanzania kwa msimu ujao katika mashindano hayo.


Lazima wajitafakari na wapige hesabu upya ili warejee kwenye mwendo wao kuendeleza ule ushindani ambao ulikuwepo awali.


Kwa upande wa Simba wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika wameishia hatua ya robo fainali na malengo yao ilikuwa ni kutinga nusu fainali. Ndoto zao zimezimwa baada ya kujiamini kupita kiasi hivyo kuna jambo wamejifunza wakati ujao wataongeza nidhamu.