Home Uncategorized HAWA HAPA NYOTA WANNE SIMBA IMEMALIZANA NAO JUMLAJUMLA

HAWA HAPA NYOTA WANNE SIMBA IMEMALIZANA NAO JUMLAJUMLA

TAYARI mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, na Kombe la FA wamemalizana na nyota wanne wa kazi ambao msimu ujao watakuwa na uzi mwekundu.


Baada ya dirisha la usajili kufunguliwa, Agosti Mosi, tayari Simba nao wameingia sokoni kuboresha kikosi kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21.


Nyota wake wanne ambao wameshasaini dili la miaka miwili ni pamoja na Ibrahim Ame ‘Varane’ akitokea Coastal Union ya mkoani Tanga, Charles Ilanfya akitokea KMC, David Kameta,’Duchu’ na Bernard Morrison akitokea Yanga.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wataendelea kufyatua vitu ndani ya mwezi huu wa usajili mpaka pale watakapoona inatosha.


“Mwezi Agosti wakati wa dirisha la usajili tutafyatuafyatua vitu na kuumiza roho za watu hivyo wasijali tupo vizuri sisi ni mabingwa na mimi ni msemaji wa timu kubwa lazima niongee kwa umakini,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA GAZETI LA SPOTI XTRA KATIKA UKURASA WA MBELE LEO ALHAMIS