Home Habari za michezo RASMI….SIMBA WAMWEKA CHAMA SOKONI…..DAU LAKE SIO POA….YANGA WATAJWA….

RASMI….SIMBA WAMWEKA CHAMA SOKONI…..DAU LAKE SIO POA….YANGA WATAJWA….

Habari za Simba SC

Endapo Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wapo tayari kumsajili kiungo mchezeshaji kutoka Zambia, Clatous Chama wametakiwa kutoa dau la dola 300,000 (zaidi ya Sh 752 Mil) ili waununue mkataba wake wa mwaka mmoja ambao ameubakisha Simba SC.

Tetesi zinasema kuwa kiungo huyo, anawaniwa vikali na baadhi ya klabu za hapa nchini kati ya hizo ni Young Africans ambaye anatajwa kwenda huko na Azam FC.

Kiungo huyo hivi karibuni alisimamishwa na uongozi wa Simba SC kutokana na utovu wa nidhamu pamoja na kiraka Nassoro Kapama ambao hawapo kambini hivi sasa.

Taarifa zinaeleza kuwa, Simba SC imekubali kumuachia kiungo huyo kwa sharti la timu husika inayomuhitaji kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja kwa dau hilo la zaidi ya Sh 700 Mil.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, uongozi wa Simba hauna utamaduni wa kumzuia mchezaji kuondoka hapo na kwenda sehemu yenye maslahi yake.

Aliongeza kuwa wanaheshimu ubora wa kiungo huyo mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za mabao, lakini kama mwenyewe akihitaji kuondoka hapo, kamwe hawatamzuia kikubwa afuate taratibu na aheshimu mkataba wake.

Ili mkataba wa Chama uvunjwe, basi klabu husika itatakiwa kutumia zaidi ya Sh 700 Mil, kama kikitoka kiwango hicho cha fedha, basi uongozi hautamzuia kuondoka hapo.

Kiwango hicho fedha kipo katika mkataba wake Chama, ili timu itakayomuhitaji kumsajili iwe ndani au nje ya nchi, basi itatakiwa kutoa dau hilo la fedha.

“Kama kiwango hicho cha fedha kitatoka, basi hatutamzuia mchezaji huyo kuondoka, kwani hiyo fedha itakayopatikana kutokana na mauzo yake yatamsajili mchezaji mwingine wa kiwango chake,” amesema mtoa taarifa huyo.

Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, SC hivi karibuni alizungumzia hilo la usajili kwa kusema kuwa “Hatima ya mchezaji kuachwa au kuuzwa lipo chini ya kocha wetu Benchikha (Abdelhak) ambaye yeye ndiyo atatoa mapendekezo ya usajili, kwani yeye ndiye anajua umuhimu wa kila mchezaji katika timu.”

SOMA NA HII  KISA YANGA...CESAR MANZOKI AWAZIMIA SIMU SIMBA....WALIKUBALINA KILA KITU GHAFLA KABADILI GIA ANGANI....