Home Habari za michezo SAUTI YA MASHABIKI SIMBA YAFIKIWA…TRY AGAIN AKUBALI YAISHE ….ANYOOSHA MIKONO JUU…

SAUTI YA MASHABIKI SIMBA YAFIKIWA…TRY AGAIN AKUBALI YAISHE ….ANYOOSHA MIKONO JUU…

Habari za Simba leo

Uongozi wa Simba SC, umesema utakutana na baadhi ya wanachama wao kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu klabu yao.

Akizungumza na Azam TV, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salum Abdallah Try Again, amesema anawashukuru mashabiki na wanachama wa Simba kwa kuendelea kuiamini klabu licha ya kutoka kupoteza mchezo dhidi ya Yanga SC lakini pia kumpoteza Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’.

Alisema kwa sasa mashabiki wa Simba kwa sasa wanatakiwa kushikamana, kujiandaa na mchezo wa ASEC Mimosas utakaochezwa Novemba 25, 2023 mchezo wa hatua ya Klabu Bingwa Afrika.

“Nilipokea email ya mashabiki wakiomba kukutana na uongozi wangu, hii kwetu ni jambo zuri sana. Nimeona barua ile imesainiwa na Ustaz Masoud, Don King, Haruna Nazi na watu kama saba nane hivi. Tumepokea maoni yao waliyoyaandika tutayafanyia kazi lakini pia kukutana nao,” alisema Try Again.

Katika hatua nyingine, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema mashabiki wao ndio watajaokuwa wageni rasmi katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25, 2023.

Ahmed ameyasema hayo alipokuwa akitangaza ratiba yao kuelekea mchezo huo mkubwa utakaopihgwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

β€œWageni rasmi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas watakuwa ni mashabiki wa Simba. Kwanza wametoka kushinda tuzo ya mashabiki bora hivyo kila Mwanasimba akija siku hiyo ajue yeye ni mgeni rasmi.”

β€œTusahau yaliyopita na tuangalie mbele. Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa tukipoteza na tukiwa nyumbani hatutakuwa kwenye sehemu nzuri ya kwenda hatua ya mbele. Twendeni tukawape moyo wachezaji wetu kwamba tunaanguka pamoja na kusimama pamoja.”

SOMA NA HII  SIMBA HAWATAKI UTANI KABISA, WENGINE WATATU WATAMBULISHWA SIO POA