Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA CAF NA WAALGERIA….MASTAA ‘WASUKWA’ KIULAYA ULAYA…

KUELEKEA MECHI YA CAF NA WAALGERIA….MASTAA ‘WASUKWA’ KIULAYA ULAYA…

Habari za Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi hataki masihara baada ya kuwapa mbinu mpya ya kufunga wachezaji wake wanapokuwa eneo la hatari la mpinzani.

Hatua hiyo ni baada ya kuwafatilia wapinzani wao na kujiandaa kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria mcheso huo utakaochezwa nchini humo Novemba 24, mwaka huu.

Kocha huyo amesema mipango yake ni kutafuta matokeo chanya katika mchezo huo wa ugenini hasa kutumia nafasi wanazozipata wanapokywa kwenye eneo la hatari la mpinzani

Amesema kutokana na mfumo anaoutumia kila mchezaji anatakiwa kufunga sio lazima asubiri mshambuliaji hasa wanapokuwa kwenye eneo la hatari la mpinzani wanaweza kupasiana na yoyote kufunga.

“Sasa hivi tumeanza hayo mazoezi pale tunapokuwa kwenye eneo la hatari, wachezaji wanatakiwa kuwa makini, tunaenda kucheza mechi ngumu yenye ushindani, wapinzani wetu wako vizuri katika kila eneo, tunahitaji kutafuta matokeo tukiwa ugenini,” amesema kocha huyo.

Amesema wachezaji wote wana kazi ya kupambania uwanjani ili kutafuta ushindi, na lazima kila mtu kuwa makini kutumia vizuri nafasi zinazopatikana bila kujali anacheza nafasi gani.

Ameongeza kuwa katika mazoezi ni kujifunza jinsi ya kuzuia wapinzani na kufunga, wanapokuwa katika eneo la hatari kutumia nafasi vizuri na kuwa makini katika kufunga.

Amesema anachohitaji ni kupata ushindi katika mchezo wa kwanza, anaamini akianza vizuri haitokuwa tabukatika michezo inayofuata.

Gamondi ameeleza kuwa wapinzani wao, CR Belouizdad, kesho wanamchezo wa Ligi Kuu ya Algeria, dhidi ya JS Kabylie, atalazimika kuwafuatilia kwa karibu kuweza kugundua zaidi mapungufu waliyonayo zikisalia siku chache kucheza nao.

Kocha huyo amesema leo ametoa mapumziko kikosi chake na kesho kitaendelea na mazoezi kuhakikisha wanakuwa sawa kuwakabili wapinzani wao na kurejea nyumbani na ushindi.

SOMA NA HII  SAA KADHAA KABLA YA KUSHUKA DIMBANI HUKO NIGER..BOCCO AIBUKA NA HILI JIPYA...AOMBA DUA...