Home Yanga SC TSHISHIMBI AFUNGUKA HAYA KUHUSU YANGA…ADAI ILIKUWA TIMU MBAYA SANA..AWATAJA WACONGO

TSHISHIMBI AFUNGUKA HAYA KUHUSU YANGA…ADAI ILIKUWA TIMU MBAYA SANA..AWATAJA WACONGO


NAHODHA wa zamani wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi yupo jijini Dar es Salaam, huku akificha kilichomleta, lakini kafungukia usajili wa chama lake la zamani akidai ni bab’kubwa na kama wapinzani wasipojipanga vyema watapata tabu sana.

Kiungo huyo aliyekuwa AS Vita iliyomsajili baada ya kuachana na Yanga msimu uliopita, amesema usajili wa nyota wapya 11 wakiwamo Wakongomani wenzake umeiimarisha timu hiyo na anaamini itafanya vyema ndani na kwenye mechi za kimataifa.

Hadi sasa Yanga imesajili nyota 11 ambao ni Djigui Diarra, Erick Johola, Djuma Shaban, David Brayson, Yannick Bangala, Khalid Aucho, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Dickson Ambundo, Yusufu Athuman na Jesus Moloko.

Tshishimbi alisema: “Kikosi sio kipya licha ya wachezaji waliosajiliwa kuwa ni wapya, ila asilimia kubwa wanafahamiana kwa vile baadhi wamecheza ligi pamoja na wengine wamekutana kwenye timu za taifa, haitakuwa kazi ngumu ya kutafuta muunganiko hasa kwa Wakongomani wenzangu.”

Kiungo huyo aliongeza kuwa hawezi kuzungumzia mchezaji mmojammoja, lakini kwa asilimia kubwa ni usajili mzuri na mkubwa kwa timu hiyo, huku akiweka wazi kuwa uzoefu wa nyota hao kwenye mashindano ya ndani na kimataifa utakuwa na chachu kubwa kikosini.

“Unajua yanazungumzwa mengi juu ya usajili huo, wengi wakisema ni kikosi kipya itakuwa ngumu kukaa pamoja muda mfupi na kuipa timu mafanikio. Sio kweli, Yanga iliyopita ilikuwa mpya na wamemaliza nafasi ya pili, hili ni suala la kocha na mbinu zake na sio upya wa wachezaji,” alisema Tshishimbi.

SOMA NA HII  RASMI : YANGA NA SIMBA KUKUTANA MOROCCO..YANGA WAFUNGUKA HAYA