Home Yanga SC RASMI : YANGA NA SIMBA KUKUTANA MOROCCO..YANGA WAFUNGUKA HAYA

RASMI : YANGA NA SIMBA KUKUTANA MOROCCO..YANGA WAFUNGUKA HAYA


Hatimaye Uongozi wa Young Africans umethibitisha Rasmi taarifa za kikosi cha klabu hiyo kuweka kambi nchinj Morocco.

Awali taarifa hizo zilisikika kama tetesi, licha ya baadhi ya wanachama na viongozi kuandika na kuzungumza katika mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya vyombo vya habari.

Mapema hii leo Uongozi wa Young Africans kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo, umethibitisha kwa kuweka taarifa rasmi ya kambi hiyo.

“Kikosi cha timu ya Wananchi kitaondoka Dar es Salaam kwenda Morocco kwa Maandalizi ya msimu ujao.” imeeleza taarifa hiyo.

Young Africans inayonolewa na Kocha Nasrideen Mohamed Nabi itakuwa kambini nchini Morocco hadi mwishoni mwa mwezi huu, na kisha itarejea nchini tayari kwa Siku ya Mwananchi Agosti 29.

Young Africans inajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ‘CAF’.

Wakati Yanga wakiweka wazi juu ya safari hio, Simba pia wameenda Morocco leo, ambapo pengine kuna uwezekano timu hizo zinaweza kukutana huko.

SOMA NA HII  YANGA NA DJUMA IMEENDA... AZUIWA KUINGIA KAMBINI.....NAFASI YAKE KUCHUKULIWA NA HUYU..