Home Habari za michezo YANGA NA DJUMA IMEENDA… AZUIWA KUINGIA KAMBINI…..NAFASI YAKE KUCHUKULIWA NA HUYU..

YANGA NA DJUMA IMEENDA… AZUIWA KUINGIA KAMBINI…..NAFASI YAKE KUCHUKULIWA NA HUYU..

Habari za Yanga SC

Juzi mchana wakati unapiga ugali wako, Yanga walikuwa wanakamilisha tukio muhimu kwao. Walikuwa wanakamilisha usajili wa beki wa kulia wa ASEC Memosas, Kouassi Yao. Lakini Djuma Shaaban ndiyo basi tena, hata kambini amezuiwa kuingia.

Muda wowote kibango cha ‘Thank You’ kitamganda. Yao pia alikuwa kwenye rada ya Simba lakini baadaye walibadili gia na kumfuata beki wao wa zamani David Kameta ‘Duchu’, kutokana na kubanwa na idadi ya wachezaji wao wa kigeni.

DJUMA AANGUA KILIO

Kama kuna siku ngumu kwa Djuma Shabaan tangu atue Tanzania basi ni juzi Zandaani kabisa kutoka kwenye ofisi za tajiri wa Yanga, katikati ya Jiji ni kwamba aliangua machozi baada ya viongozi kumkazia kwamba lazima asepe.

Kama ambavyo ilifahamika wiki hii kwamba ujio wa Yao ni mahususi kuchukua nafasi ya Soja ya Bemba ambaye mwendo ameumaliza katika maisha ndani ya klabu hiyo.

Djuma licha ya kufika kwa wakati nchini kuja kuanza msimu mpya amekutana na zuio la kutoingia kambini baada ya mabosi wa Yanga kujihakikishia kumnasa Yao ambaye amekuja kwa mapendekezo ya Gamondi.

Kocha Gamondi amehitaji beki wa kulia anayejua kupandisha mashambulizi kwa kasi kisha kurudi kuzuia haraka wakati timu yake inapopoteza mpira na Yanga kuona mtu muafaka ni Yao.

Djuma wakati wowote kuanzia leo atapewa mkono wa kwaheri ndani ya klabu hiyo na huenda akatua TP Mazembe ya Lubumbashi kwani Azam iliyokuwa ikitajwa kumuwania tayari imeshamfungia vioo na Simba hakuna nafasi.

Mbali na kiwango chake duni chake kuchuja lakini pia alikuwa akishutumiwa kuwa na matatizo ya nidhamu ndani ya klabu hiyo hatua ambayo imechangia kusitishiwa mkataba wake na inadaiwa pia Gamondi amejiridhisha pia kwa kuzungumza na Nabi Mohammed na timu yake.

SOMA NA HII  BARCELONA YAMPIGIA HESABU HAALAND KISA MESSI