Home Ligi Kuu LEO NI BIASHARA UNITED V NAMUNGO

LEO NI BIASHARA UNITED V NAMUNGO


 LEO Uwanja wa Biashara Mara kutakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Biashara United v Namungo, utakaochezwa Uwanja wa Karume, Mara saa 10:00 jioni.

Mshindi wa mchezo wa leo atacheza hatua ya nusu fainali na mshindi wa mchezo kati ya Yanga v Mwadui ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kambarage, Jumanne.

Ofisa Habari wa Biashara United, Idrissa Sechombo  amesema kuwa kila kitu kipo sawa.

“Maandalizi yapo sawa na wachezaji wana morali kubwa hivyo ni suala la muda katika kutafuta ushindi, mazoezi ya mwisho tumefanya.

“Tulifika jana Musoma tukitokea Dar na kufanya mazoezi mepesi jana hiyohiyo, mashabiki watupe sapoti,”.


SOMA NA HII  BIASHARA UNITED YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA