Home Uncategorized NI MUDA WA KLABU ZOTE BONGO KUUNGANA KWENYE VITA HII, ILE VITA...

NI MUDA WA KLABU ZOTE BONGO KUUNGANA KWENYE VITA HII, ILE VITA YA AWALI MUDA WAKE UMEISHA


VITA ni vita bila kujali ni jambo la aina gani ambalo unapambana nalo kikubwa ni mpango mpya na kujua namna ya kuingia kwa hesabu kutafuta ushindi.

Hakuna jambo lenye mwanzo ambalo likakosa mwisho hamna kitu kama hicho ila cha msingi ni kuendelea kupambana kwa kadri unavyoweza bila kuchoka.
Mambo yanazidi kuwa magumu kwa sasa lakini hii inatokana na namna unavyozidi kupambana kutafuta matokeo ya kile unachokitaka.
Hakuna namna ya kufanya kwa sasa zaidi ya kuendelea kuomba dua kwa Mungu atufanyie wepesi kwenye janga hili ambalo tunapitia kwa sasa.
Virusi vya Corona ni wimbo wa taifa na dunia nzima kiujumla ninaamini kwa sasa wengi wana hofu kubwa na wanashindwa kujua kipi cha kufanya.
Kitu cha msingi kwa sasa kila mmoja ni kuchukua tahadhari kwa kujilinda yeye mwenyewe pamoja na jamii ambayo inamzunguka ili awe salama.
Ukiwa salama wewe maana yake ni kwamba unaongeza idadi ya wale ambao watakuwa salama kutoka kwenye maambukizi mapya ambayo yapo kwa sasa.
Inauma kuona ndugu jamaa na marafiki wanatangulia mbele za haki kutokana na Virusi hivi vya Corona lakini tunapaswa tushukuru katika kila jambo.
Mungu wetu pekee anajua namna atakavyotuokoa kutoka kwenye janga hili tumtumaini yeye pekee anaweza yote bila mashaka yoyote.
Hakuna jambo ambalo analishindwa kwa kuwa yeye ndiye muumba wa yote anapaswa kushukuriwa na kuheshimiwa pia.
Bado ninaongea na wale ambao hawajali na wanaendelea na shughuli zao bila kuchukua tahadhari hiyo sio sawa hata kidogo.
Maombi yangu kwa wale ambao hawana mpango wa kusafiri ama kutoka nje wawe mabalozi wazuri kwa sasa ndani ya nyumba zao ili kuokoa wengine wasiingie kwenye mnyororo wa janga hili.
Wale ambao bado hawajaanza kuchukua tahadhari ni wakati wao wa kufanya hivyo ili kuwa salama kwa kiasi chake kwani kinga ni bora kuliko tiba.
Wizara ya afya imekuwa ikitoa mrejesho na taarifa mara kwa mara kuhusu namna ya kujilinda na kuchukua tahadhari ni muhimu kufuata utaratibu unaotolewa na Serikali.
Kuna ishu ya kuvaa barakoa pia kwa wale ambao wanaingia kwenye ofisi kupata huduma ni muhimu kufuata taratibu hizo ili kuwa salama zaidi.
Kikubwa kitakachotuvusha salama hapa ni kufuata utaratibu uliowekwa na kuwa makini kwenye kujali afya zetu ambazo ni mtaji mkubwa wa kwanza.
Wapo ambao bado hawaamini kama ugonjwa huu upo mtaani kutokana na kuishi kawaida na shughuli zao kuendelea kama ilivyokuwa kawaida.
Hiyo sio sawa muhimu kufuata maelekezo ya Serikali na kufuata kanuni za afya ili kujilinda sisi wenyewe hii vita tumeanza ni lazima tuimalize kwa pamoja.
Asiwepo wa kubaki nyuma katika hili kwani dunia itamshangaa yule ambaye atashindwa kuungana nasi kupambana na vita hii mpaka pale mambo yatakapokuwa sawa.
Tunaona kwa sasa watoto wapo nyumbani wakiendelea kusubiri tamko la Serikali kurudi shule kuendelea na masomo nao pia wanapaswa wafuate kanuni.
Ulinzi wa mtoto unapaswa uwe mkubwa ili pale atakaporejea shule awe na afya ya kutosha na uwezo wa kuendelea kupambania ndoto zake.
Pia ni wakati wa timu zote Bongo kuungana katika vita hii ili kutengeneza dunia yao nyingine kwa kuacha ule uhasama ambao wanakuwa nao hasa wanapokutana uwanjani.
Ipo wazi kwamba vita ya mpira ni ndani ya dakika tisini ambazo ni zile za uwanjani na sio namna nyingine tena.
Baada ya dakika tisini kukamilika kinachofuata ni ushirikiano na kila mmoja kuwa ni familia moja na kufanya kazi kwa ushirikiano ndio maana wachezaji walikua wanapeana mikono na wakati mwingine wanabadilishana jezi pia.
Basi kwa wakati huu ni sahihi kuungana pamoja kuanza kazi upya ya kuongeza nguvu kupambana na Virusi vya Corona kwa vitendo.
Tunaona kwamba hivi karibuni Klabu ya Pamba ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ilianza kutoa sapoti kwa kuwatembelea wale wenye mahitaji maalumu.
Pamba SC wao walianza kwa kutembela Kituo Cha Watoto wenye Uhitaji maalumu cha kulea na kuwasaidia watoto waliofanyiwa ukatili cha Foundation Karibu Tanzania kilichopo Kiloleli Jijini Mwanza.
Hapa pana kitu cha kujifunza kwao kwani wamefungua njia ili klabu nyingine pia zifuate katika kupambana na Virusi vya Corona.
Licha ya kwatembelea wahitaji pia Pamba ilipata muda wa kujenga mahusiano mapya na kuwa familia inayojali kwa kugawa vitakasa mikono yaani Sanitizer kwa kila motto.
Hatua hii ni kubwa na ina kitu cha kipee ambacho ni darasa kwa kila mmoja, ninaona kwamba iwapo wengine wataiga kwa vitendo itakuwa vyema kuzidi kufungua ulimwengu wa kuendelea kupambana na Virusi vya Corona.
Bado nafasi ipo kwa sasa haina maana kwamba ni lazima iwe kwa makundi hapana dunia imebadilika na teknolojia imekuwa kubwa.
Kuna namna ambayo uongozi wa timu unaweza kufanya na wengine wakafuata hesabu hizo kwa kujadiliana namna ambavyo wanaweza kusaidia jamii.
Inaweza kuwa kwenye mitandao ya kijamii ama kupitia email ambapo timu zinaweza kuamua namna bora ambayo itawafanya waweze kujadili kuungana na Serikali.
Vita ya kwenye Istagram na mitandao ya kijamii pekee bila vitendo kwa sasa muda wake umekwisha hiyo ilikuwa pale awali wakati mapambano yanapoanza.
Kwa sasa kwa viongozi wa timu ni wakati wa kubadili aina ya silaha ya kupambana na Virusi vya Corona ile ya kwanza tayari muda wake umekwisha.
SOMA NA HII  KUMEKUCHA, YANGA YACHARUKA, YAISHITAKI SELCOM KWA SERIKALI