Home Uncategorized KUMEKUCHA, YANGA YACHARUKA, YAISHITAKI SELCOM KWA SERIKALI

KUMEKUCHA, YANGA YACHARUKA, YAISHITAKI SELCOM KWA SERIKALI



Uongozi wa Yanga umeishtaki Kampuni ya Selcom Tanzania, serikalini kutokana na utendaji wao wa kazi mbaya ambao ulikuwa wa wizi na rushwa uliotokea kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.


Kilele hicho cha Wiki ya Mwananchi kilikuwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa timu hiyo kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Kariobang Shark’s ya Kenya na Yanga kwa timu hiszo kutoka sare ya bao 1-1.



Akizungumza na Waandishi wa Habari, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa hawakuridhishwa na utendaji kazi wa Selcom ambao kama ukiendelea, basi serikali utapoteza mapato mengi.


Mwakalebela alisema kuwa mawakala wa kampuni hiyo ndiyo walikuwa tatizo waliokuwa wanauza tiketi mara mbili kwa mashabiki waliokuwa wamejitokeza.


“Leo Jumatatu tunatarajia kuandika barua kwenda serikalini kwa ajili ya kuwataarifu wizi na rushwa iliyokuwa inafanyika katika kilele chetu cha Wiki ya Mwananchi.


“Kikubwa tunataka kuwafahamisha tatizo hilo lililotokea siku hiyo ya tukio na mbaya zaidi siku hiyo tiketi za Simba Day zilizopangwa kutumika kesho zimetumika kwenye tamasha leu, hivyo tunashinda kufahamu hizo pesa zinakwenda Simba au Selcom,” alihoji Mwakalebela.

SOMA NA HII  LIIVE!! TOWNSHIP ROLLERS 0-0 YANGA, LIGI YA MABINGWA AFRIKA