Home Yanga SC BAADA YA KUSAJILI WACONGO WENGI..YANGA WAAMUA ‘KUTOMBOKA’ NA KOFFI OLOMIDE SIKU YA...

BAADA YA KUSAJILI WACONGO WENGI..YANGA WAAMUA ‘KUTOMBOKA’ NA KOFFI OLOMIDE SIKU YA MWANANCHI


MSANII wa muziki aina ya dansi, Koffi Olomide atakuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza katika siku ya Mwananchi itakayofanyika Agosti 29 katika Uwanja wa Mkapa.

Mwenyekiti wa kamati ya habari na hamasa na mjumbe wa kamati ya utendaji Yanga, Suma Mwaitenda alisema kwenye tamasha hilo licha ya kuwa na wasanii wengi ila wataongozwa na Koffi Olomide.

“Tutakuwa na Namba ambayo itakuwa inaweka statasi kwenye simu na kuonyesha kila ratiba ya tukio itakavyokuwa, hii ni timu ya wananchi na namba hii itawasaidia wanachama kupata ratiba,” alisema Mwaitenda.

Viingilio katika siku ya Wananchi kwa chini itakuwa ni shilingi elfu tatu (3000) na kiwango cha juu ni shilingi laki mbili (200000) ambao watakuwa na uangalizi mwingine.

SOMA NA HII  YANGA YAINGIA ANGA ZA MSHAMBULIAJI HUYU, KUCHUKUA MIKOBA YA NTIBANZOKIZA