Home Yanga SC BAADA YA KUSIMAMISHWA..NIYONZIMA AVUNJA UKIMYA YANGA..

BAADA YA KUSIMAMISHWA..NIYONZIMA AVUNJA UKIMYA YANGA..


KIUNGO fundi wa mpira wa Yanga, Haruna Niyonzima amevunja ukimya baada ya sintofahamu iliyojitokeza kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba.

Niyonzima ameunguliwa katika kambi hiyo kwa utovu wa nidhamu akiwamo beki Lamine Moro na Michael Sarpong na hawatakuwa kwenye kikosi cha Yanga leo dhidi ya Simba katika Ligi Kuu Bara baada ya mechi hiyo kuahirishwa Mei 8.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Niyonzima alisema anashindwa kuelewa utovu wa nidhamu aliouonyesha kwani alikuwa anaumwa na kusababisha kukosekana katika safari ya mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Shirkisho dhidi ya Biashara United mkoani Tabora.

“Nilikuwa ninaumwa na dozi yangu ya dawa ilimalizika Jumatatu, siku iliyofuata nilikuwa niingie kambini, lakini wakati najiandaa kwenda nilipata ujumbe sitakiwi kwenda na sitakuwepo kwenye mipango ya mechi ya Jumamosi,” alisema Nyonzima.

Alisema baada ya taarifa hiyo alihoji sababu ni zipi, lakini hakupata jibu, hivyo akaona ni busara kukaa kimya na kuendelea kujisikilizia ili mwili wake uwe fiti zaidi kama awali.

“Mpira ni kazi yangu naipenda, siwezi kuifanyia masihara hata siku moja, halafu mi sio muongeaji na sipendi kuongea ila kila jambo linalotokea ni mipango ya Mungu kwani ndiye ninayemwamini na kumtukuza.”

Mkuu wa Idara ya Habari ya Yanga, Hassan Bumbuli alipotafutwa juu ya utetezi wa kiungo huyo alisema kwa kifupi; “Kwa sasa tuko bize sana na maandalizi ya derby.”

SOMA NA HII  YANGA YAWEKA REKODI HII MPYA...HAKUNA TIMU ILIYOWAHI...AFRIKA YATETEMA