Home Habari za michezo KAMWE:- KWA HIZI 5G….WALIOSAJILI ‘JOBLESS NA FREDY VUNJA BEI’ WAJIANDAE NA KULA...

KAMWE:- KWA HIZI 5G….WALIOSAJILI ‘JOBLESS NA FREDY VUNJA BEI’ WAJIANDAE NA KULA 10G..

Habari za Yanga

Ofisa Habari wa Klabu ya yanga, Ally Kamwe amesema kuwa, kabla msimu huu haujamalizika, ana uhakika kuna timu wataifunga mabao 10 kwenye mchezo mmoja.

Kamwe amesema hayo baada ya kumaliza deni lao na timu ya Ihefu FC ambapo jana Jumatatu, Machi 11, 2024, waliifunga mabao 5-0 katika Dimba la Azam Complex.

Itakumbukwa kuwa, Ihefu ndiyo timu iliyofungwa na Yanga bao 2-1 msimu uliopita na kuiharibu unbeaten yao ya 49 kuelekea 50. Isitoshe, msimu huu, Ihefu ndiyo timu pekee ambayo imeifunga Yanga kwenye michezo yake yote 18 ambayo imecheza, hivyo Wananchi walikuwa na kila sababu ya kulipa kisasi hicho.

“Chukueni maneno yangu mtakuja kuniuliza, hii dozi ninawaambia kuna mtu atakula bao 10 kabla msimu huu haujaisha, kama sio hapa basi kwenye uwanja wake atakaochagua kuchezea, 10 zinakuja, hawa wanaokuja hapa mbele wapeni salam.

“Hizi 10 zitamkuta yeyote aliyechezacheza kwenye usajili na waliouza timu. Ukija kucheza na Yanga kama umeshauza timu na hujui kama umeuza, basi ujiandae.

“Kama sisi wakati tumasajili Okrah Magician, Guede na Shekhan Ibrahim wewe unaenda kuleta Jobless na Fredy Vunjabei, bao 10 zipo, hapa tunatafutiana lawama,” amesema Ally Kamwe.

Mpaka sasa, Yanga imefunga timu nano mabao matano matano kwenye mchezo mmoja mmoja msimu huu;
◉ Yanga 5 – 0 KMC
◉ Yanga 5 – 0 JKT Tanzania
◉ Yanga 5 – 1 ASAS
◉ Yanga 5 – 1 Simba SC
◉ Yanga 5 – 0 Jamhuri
◉ Yanga 5 – 1 Hausing FC
◉ Yanga 5 – 0 Polisi Tanzania
◉ Yanga 5 – 0 Ihefu FC.

Mechi inayofuata ni Yanga dhidi ya Geita Gold FC.

Pengine Miguel Gamondi ndiye kocha katili zaidi kwenye historia ya Yanga SC?

SOMA NA HII  KOCHA TAIFA STARS ALIVYOBADILI UPEPO WA MASHABIKI WA BONGO KUHUSU TIMU YA TAIFA...