Home Uncategorized ALLIANCE FC KUIFUMUA SIMBA NA YANGA

ALLIANCE FC KUIFUMUA SIMBA NA YANGA

UONGOZI wa Alliance FC ya mkoani Mwanza umesema kuwa msimu ujao lazima wawe moto hasa kwa kuwapata wachezaji wenye uzoefu watakoongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Alliance walianza kwa kusuasua msimu huu kabla ya kufanya maboresho kwenye kikosi chao kwa kuleta wachezaji wenye uzoefu pamoja na mabadiliko ya benchi la ufundi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Alliance, Jackson Mwafulango amesema kuwa wameamua kuanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao mapema ili kuleta mapinduzi kwenye soka.

“Unajua Alliance kazi yetu msimu huu ilikuwa ni kusambaza misumari ya upendo sasa tumejipanga msimu ujao kuanza maboresho ndani ya kikosi kwa kuleta wachezaji wenye uzoefu ili kuzidisha ushindani.

“Tunajua kuna wachezaji kutoka Simba, Yanga ambao wana uwezo na uzoefu hivyo kama ripoti ya mwalimu itampendekeza mchezaji kutoka huko tunafanya naye mazungumzo” amesema Mwafulango.

SOMA NA HII  DOZI YA KMC KUIWINDA AS KIGALI NI MARA MBILI KWA SIKU