Home Uncategorized YANGA KUMALIZANA NA BEKI KISIKI WA KMC

YANGA KUMALIZANA NA BEKI KISIKI WA KMC


IMEEELEZWA kwamba uongozi wa Yanga umeanza mazungumzo na beki wa kikosi cha KMC, Ally Ally ‘Mwarabu’ ili kupata saini yake msimu ujao.

Mwarabu amekuwa kiongozi ndani ya KMC na kuifanya safu ya ulinzi kuwa kisiki kwani KMC imekuwa ni namba moja kwenye timu zilizotoa sare nyingi ikiwa imefanya hivyo mara 16 msimu huu.

Habari zimeelezwa kuwa Yanga tayari wamefikia sehemu nzuri ya maelewano na beki huyo ambaye ni mwepesi akiwa ndani ya uwanja.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa suala la usajili lipo mikononi mwa kocha mkuu, Mwinyi Zahera hivyo kama jina lake lipo litafanyiwa kazi.

“kama jina lake lipo kwenye orodha ya mwalimu inawezekana tukazungumza naye ila kwa sasa hakuna taarifa kamili,” amesema.

SOMA NA HII  MBELGIJI WA SIMBA ATEGUA MTEGO WAKE KIMTINDO