Home Uncategorized ISINGEKUWA CORONA WANGETENGENEZA MKWANJA MREFU KINOMA HAWA JAMAA

ISINGEKUWA CORONA WANGETENGENEZA MKWANJA MREFU KINOMA HAWA JAMAA

LABDA kwa sasa wangekuwa wanakenua huku akaunti zao zikiwa zimevimba mkwanja wa kutosha kutokana na kufanya shoo ambazo zingewaingizia mtonyo mrefu nje na ndani ya Bongo.
Ngoma zao ni kali na zinapendwa kwa sasa ila Virusi vya Corona vimetibua kwa upande wa shoo wanaishia kuambulia malipo kutoka YouTube.
Kutokana na ukali wa kazi zao, bila shaka wangekuwa wameshapata mialiko mbalimbali ya kwenda kupiga shoo katika mikoa na nchi mbalimbali.
Makala hii inakuangazia baadhi ya kazi za wasanii wa kibongo ambao kazi zinafanya poa redioni, kwenye televisheni, mtaani na kwenye ‘Media Platforms’
Diamond
Thamani ya Diamond Platnumz ni kama lilivyo jina lake. kwenye muziki, ukitaja watu watatu wanaokimbiza Bongo kwa sasa, huwezi kuliacha jina lake. 
Ziara yake nje ya nchi huko Ufarasa ilikatishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona na aliporudi Bongo karantini ilimhusu huku meneja wake Sallam SK akitangaza kupitia Ukurasa wake wa Istagram kuwa ameathirika na Virusi vya Corona.
Kwa sasa hapokei tena simu za shoo kama ilivyokuwa awali kwa sababu hakuna nchi ambayo inafanya shughuli yoyote ya kiburudani. Ngoma ya mwisho kuitoa ilikuwa ni Jeje, Februari 25, mpaka sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni 13 huko Youtube.
Kibwagizo:”I go fight like John Cena, ni moja ya kibwagizo kinachoipamba ngoma hiyo, iliyowahi kukaa Youtube trending kwa zaidi ya siku nne.

Ali Kiba
Anatamba na mkwaju wa Dodo, ulitoka April 8, ni moja ya ngoma kali kwa sasa mjini na imesumbua sana Youtube Trending, uwepo wa Hamisa Mobeto umeongeza ubora wa video hiyo.
Mwaka umekuwa mzuri kwa King Kiba, pengine isingekuwa  Corona tungesikia naye anakula mwewe na kwenda kupiga mashoo kibao huko mbele, sema ndiyo hivyo tena Corona imevuruga mipango.
Ngoma imegonga Views Zaidi ya milioni tatu Youtube pengine ndiye huko pekee atakuwa anakinga mkono na kuvuta mkwanja na siyo kusimama jukwaani kama ilivyokuwa kawaida ya wasanii wengi wa Bongo.
Marioo
Mwaka jana ulikuwa wake, hata mwaka huu pia unaonekana kuwa vizuri vilevile. Sauti kali yenye mpangilio mzuri akiwa anaimba inatosha kueleza kuwa ni miongoni mwa wasanii ambao hawachoshi kuskilizwa na kuwatazama.
Ukisikliliza Inatosha, Aya, Unanikosha, na mikwaju mingine, ungetamani kumuona akiperform jukwaani, lakini itabidi atulie kwanza, kama hana chanzo kingine cha mapato kwa sasa anaweza kushika spana na kurudi gereji kurudia fani yake. Maana Corona imetibua kila kitu.
Darassa
Ngoma ya Darassa akiwa na mrembo Sho Madjozi imepandishwa kwenye akaunti ya YouTube, Februari 25 na imetazamwa na watu zaidi ya milioni moja Youtube. Kwa marapa wa Bongo ni miongoni mwa nyota anayekubalika.
Mkono wa fundi ambaye huwa hakosei sana ila kidogo tu Abbah Process  na kichupa kikiongozwa na Yoza Mnyanda ni bonge moja ya ngoma.
Imesumbua kwenye vituo vya TV na radio kwa kusugua namba moja kwa mwezi Aprili na bado inatesa.
Lakini licha ya kutesa huko, hawezi kuvuta mtonyo kwa shoo zaidi ya Youtube na vyanzo vingine vya kuuza mziki mtandaoni.
Nandy
Ilikuwa Februari 28 ngoma yake Na nusu ilipandishwa kwenye akaunti ya YouTube na imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja. Sauti ya ndege manna huyu ni balaa na nusu.
Kichupa kikali kinamitego flani ya kishkaji ila ndo ishakuwa sasa huenda isingekuwa Corona angekunja mkwanja mrefu kwa kupiga shoo za maana nje na ndani ya nchi kama ambavyo alifanya mwaka uliopita.
Harmonize
Harmonize ambaye kwa sasa ni bosi wa lebo ya Konde Music World Wide, baada ya kutoa album yake ya Afro East kilichokuwa kinafuata ni mishoo na mialiko kibao ya matamasha kutoka ndani nan je ya nchi.
Kwa sababu album inatembea na kufanya vizuri sokono, lakini hawezi kupiga tena mitonyo kupitia shoo kutokana na katazo lililowekwa na Serikali.
Lakini bila shaka atakuwa anaingiza mtonyo wa kutosha kupitia Youtube, kwa sababu ni moja ya wasanii ambao wanatengeneza Views wa kutosha kupitia kazi zao.
Meja Kunta na Lava Lava
Wanga yake Meja  Kunta akiwa na Lava Lava zao la WCB imekutana na majanga makubwa matatu, msanii Kunta alibatizwa jina la marehemu anayetembea baada ya habari kusambaa kuwa amefariki kwa ajali.
Pia alikuwa na tamasha kubwa la usiku wa Kwio pale Dar Live Mbagala likayeyuka na tatu ndo kwanza Meja alikuwa anafungua ufalme wake ndani ya kisingeli kutokana na mambo kuanza kujipa ila ndo mambo yamezima ghafla.
Itabidi aendelee kufanya kazi kwa bidii huki akiwa anasubiri kuona kama mambo yanaweza kukaa sawa na ishu za kiburudani kurejea tena kama kawaida.

SOMA NA HII  KMC: HATUKUPANGA KUAMBULIA POINTI MOJA TULITAKA POINTI TATU