Home Habari za michezo AHMED ALLY:- AZAM FC HAWAJATUFUNGA KWA BAHATI MBAYA…WAMEKUWA KIKWAZO SANA KWETU..

AHMED ALLY:- AZAM FC HAWAJATUFUNGA KWA BAHATI MBAYA…WAMEKUWA KIKWAZO SANA KWETU..

Habari za Simba SC

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Kalbu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa timu yao imefungwa na Azam FC si kwa bahati mbaya bali wapinzani wao hao walikuwa bira sehemu zote na walijiandaa vizuri kuhakikisha wanapata ushindi mbele ya Mnyama.

Ahmed amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Azam FC, mkoani Mtwara ambapo Azam waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Simba na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo.

“Niwapongeze Azam FC wamekuwa na mchezo mzuri leo na hatimaye kupata ushindi. Msimu huu katika mashindano yote ya ndani Azam amekuwa kikwazo kwetu, kwenye ligi tumepoteza alama tano, shirikisho ametutoa kwenye nusu fainali.

“Kama Simba Sc tumeumia sana, Azam hawajafanya hili kwa bahati mbaya, mzimu mzima tumekutana mara tatu, wametufunga mara mbili tumetoa sare mara moja. Leo Simba hatukuwa bora ikilinganishwa na Azam, wametumia madhaifu yetu kupata ushindi na kwenda fainali.

“Azam alifanyia kazi mapungufu yake kwa miaka nane tangu achukue ubingwa huu, amepata majibu na mwisho wa siku ametuadhibu leo,” amesema Ahmed.

Azam sasa watakutana na mshindi wa nusu fainali ya pili kayi ya Yanga na Singida Big Stars ambapo mchezo wa fainali utapigwa

SOMA NA HII  SIMBA SC 'WAICHAKATA' GWAMBINA FC NA KUKALIA USUKANI WA LIGI