Home Uncategorized HATMA YA EYMAEL KOCHA WA YANGA IMESHIKILIWA NA SERIKALI

HATMA YA EYMAEL KOCHA WA YANGA IMESHIKILIWA NA SERIKALI


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unasubiri kupewa ruhusa tu kutoka kwa Serikali ya kuruhusu Ligi Kuu Tanzania Bara ili kumtumia Kocha Mkuu Luc Eymael, tiketi ya ndege ili arudi Bongo.

Eymael kwa sasa yupo nchini Ublegiji ambako alikwenda baada ya ligi kusimamishwa Machi 17 kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia.

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema:”Tunasubiri go ahed ya Serikali kuhusu kuirejesha rasmi ligi tuwatumie tiketi makocha wetu walio nje ya nchi waje haraka kuendelea na maandalizi kabla ya michuano kuanza.”

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 27 kibindoni ina pointi 51.

SOMA NA HII  BEKI YANGA AINGIA ANGA ZA COASTAL UNION