Home Uncategorized MCHAKATO WA KURUDISHA LIGI UTAANZA NAMNA HII

MCHAKATO WA KURUDISHA LIGI UTAANZA NAMNA HII


WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema wataanza kuirudisha ligi ya mpira wa miguu baada ya kufunguliwa kwa shughuli za Michezo kutokana na hali ya ugonjwa wa Corona kuzidi kutengemaa nchini.

Jumapili Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli aliweka wazi kuwa anafikiria kuruhusu shughuli za Michezo na kufungua vyuo kama hali ya ugonjwa wa Corona itazidi kutengemaa kuanzia wiki iliyoanza Jumatatu.

Mwakyembe amesema mara tu shughuli zenye mikusanyiko zitakapo ruhusiwa wataanza na soka huku michezo mingine ikifuatiwa baadae kwa kufuata tahadhali zote zinazotolewa na Wizara ya Afya. 


“Rais wa nchi amesema anafikiria kuruhusu shughuli za Michezo siku chache zijazo kama hali ya ugonjwa wa Corona itaendelea kubaki kuwa nzuri kama ilivyo sasa ila hatutaanza na Michezo yote tutaanza na soka kwanza na baadae mingine itafuata lakini tahadhali zote zitafuatwa,” alisema Dk. Mwakyembe.

SOMA NA HII  LUKAKU AKISEPA TU UNITED HAWA HAPA KUVAA VIATU VYAKE