Home Habari za michezo SIMBA QUEENS KUANZA KUUSAKA UBINGWA WA LIGI YA MABINGWA AFRIKA ‘WANAWAKE’ KWA...

SIMBA QUEENS KUANZA KUUSAKA UBINGWA WA LIGI YA MABINGWA AFRIKA ‘WANAWAKE’ KWA KUCHEZA NA HAWA….


Timu ya Simba Queens itaanza kibarua chake cha kwanza kwenye michuano ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati (CECAFA) kwa kucheza na GRFC ya (Djibouti) Agosti 14.

Simba Queens iliyopo kundi B katika michunao hiyo itaanza mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Baada ya mechi hiyo itacheza na SHE Corporate WFC kutoka Uganda Agosti 15 na kisha kumalizia kundi hilo kwa kucheza na YEI Joint Stars ya Sudan ya Kusini Agosti 18.

Mashindano hayo ambayo yanafanyika jijini Dar es Salaam yanashirikisha timu za, Simba Queens (Tanzania), Commercial Bank FC (Ethiopia), Warriors Queens FC (Zanzibar), Fofila PF (Burundi), AS Kigali WFC (Rwanda), Garde Republicaine FC (Djibouti), SHE Corporates (Uganda) na YEI Joint Stars FC ya Sudan Kusini.

Michuano hii inategemewa kuleta upinzani mkali kutokana na ubora wa timu zote zinashoshiriki yataanza Agosti 14 hadi 28

SOMA NA HII  KUHUSU MIQUISSONE KUVAA TENA JEZI YA SIMBA....'UPDATE' YA DILI LAKE HII HAPA...