Home Habari za michezo MBRAZILI SIMBA AANZA ‘KUINGIA UBARIDI’ KUKUTANA NA AL AHLY MPYA…

MBRAZILI SIMBA AANZA ‘KUINGIA UBARIDI’ KUKUTANA NA AL AHLY MPYA…

Habari za Simba SC

Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ amesema anaiheshimu Al Ahly ya Misri, hivyo hana budi kujipanga kupambana nayo katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali wa African Football League.

Simba SC itaikaribisha Al Ahly Ijumaa (Oktoba 20) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kwa mchezo huo, kabla ya miamba hiyo kurudiana katika mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa mjini Cairo Oktoba 24.

Robertinho ambaye tayari ameshaanza Programu za kujiandaa na mchezo huo, amesema Al Ahly ina wachezaji wengi wenye uzoefu mkubwa katika michuano ya Kimataifa ndani ya nje ya Bara la Afrika, hivyo ana kazi kubwa ya kufanya kukabiliana nayo.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil amesema kutokana na ugumu na umuhimu wa mchezo huo, amejizatiti kwa kuhakikisha wachezaji wake wanakuwa tayari kimwili na kiakili kupambana na miamba hiyo ya Misri, ambayo inashikilia taji la Barani Afrika.

“Hatuna budi kuwaheshimu Al Ahly, ni timu kubwa ambayo ina wachezaji wengi wenye uzoefu wa michuano ya Kimataifa ndani na nje ya Bara la Afrika, nitahakikisha tunapambana nao kwa kupata matokeo mazuri katika mchezo wa hapa nyumbani na hata kule Misri.”

“Tumeanza maandalizi ya mchezo huo, Wachezaji wangu wameonesha kuwa tayari kwa kupambana, nitahakikisha ninashirikiana na wenzangu katika benchi la ufundi ili kufanikisha malengo tuliojiwekea.”amesema Kocha Robertinho

Wakati huo huo Kesho Jumamosi (Oktoba 14) Simba SC inatarajia kucheza mchezo wa Kirafiki katika Uwanja wake wa Mazoezi wa Mo Simba Arena uliopo Bunju jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mpambano dhidi ya Al Ahly.

SOMA NA HII  KUELEKEA YANGA vs SIMBA KESHO....HAYA HAPA UNAYOPASWA KUJUA KABLA YA MECHI...