Home Uncategorized PAPE GUEYE AWEKWA KWENYE RADA ZA WATFORD

PAPE GUEYE AWEKWA KWENYE RADA ZA WATFORD


PAPE Gueye, nyota wa timu ya Le Havre AC amewekwa kwenye rada za Klabu ya Watford ambayo imeonyesha nia ya kupata saini yake kwenye usajili wa majira ya joto Ulaya.

Kiungo huyo amekubali mkataba wa awali wa mabosi hao na kinachosubiriwa ni kufanyiwa vipimo ili kujua hali yake.

Wakala wa mchezaji huyo, Pierre-Henri Bovis amesema kuwa kila kitu kuhusu mchezaji huyo kujiunga na Watford kinakwenda sawa ni suala la kusubiri msimu kukamilika.

Kiungo huyo mwenye miaka 21 anayevaa jezi namba 24 tangu msimu wa 2017/20 ndani ya Le Harve amecheza jumla ya mechi 39. 


“Kila kitu kinakwenda sawa, hakuna jambo ambalo linakwenda tofauti, kuna mipango mingi ya kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na hili la Watford, “.

SOMA NA HII  LIVE: TAZAMA HAPA CEO MPYA SIMBA AKITAMBULISHWA - VIDEO