Home Habari za michezo NTIBAZONKIZA AANZA NA MGUU WA KULIA SIMBA SC…’AKICHAFUA ILE ILE’ MAZOEZINI…

NTIBAZONKIZA AANZA NA MGUU WA KULIA SIMBA SC…’AKICHAFUA ILE ILE’ MAZOEZINI…

Habari za Simba

Hatimaye kwa mara ya kwanza kiungo mshambualiaji wa Simba SC Saido Ntibazonkiza leo amejumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya jioni ikiwa ni siku moja toka atangazwe.

Saido ambaye niusajili mpya na wa kwanza kwa Simba SC toka kufunguliwa kwa dirisha doho la usajili tarehe 15 mwezi huu, amejiunga na timu hiyo ambayo iko Mwanza ikijiandaa kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC hapo kesho.

Zifuatazo ni sehemu ya picha za tukio hilo, ambapo zinamuonyesha Saido akiwa na furaha kujiunga na Simba SC akiwa ni sehemu ya wachezaji wachache wa kigeni ambao wamepata nafasi ya kucheza Simba na Yanga .

Saido Ntibazonkiza akisalimiana na Kibu Denis leo kwenye mazoezi ya Simba SC
Saido Ntibazonkiza akionyesha ufundi mbele ya Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda

Kulingana na mazoezi ya leo, huenda kesho Kaimu Kocha MKuu wa Simba , Juma Mgunda akashawishika kumuanzisha katika kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya KMC.

Saido Ntibazonkiza akipokea maelekezo ya kiufundi kutoka kwa Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda

Saido Ntibazonkiza amejiunga na Simba  akitokea Geita Gold FC kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu,awali mchezaji huyo ambaye pia ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi aliwahi pia kuichezea Yanga  kabla ya kutemwa kwa kile kilichosemekana kuwa ni ukosefu wa nidhamu.

SOMA NA HII  HAMNA HAMNA ...YANGA WANAWEZA KUPANGWA KUKIPIGA NA HAWA ROBO FAINAL YA CAF...