Home Habari za michezo NABI AGOMA KISA FEI TOTO….ATOA MAELEZO HAYA KWA MASTAA YANGA SC..

NABI AGOMA KISA FEI TOTO….ATOA MAELEZO HAYA KWA MASTAA YANGA SC..

Habari za Yanga SC

Wakati sakata la kiungo Feisal Salum likishika kasi kocha wa Yanga Nasreddine Nabi amegoma kuzungumzia ishu hiyo akisema anataka ushindi kwanza dhidi ya Azam.

Nabi amesema kiungo huyo ambaye amekacha kambi yao kuanzia Ijumaa kujiandaa dhidi ya Azam hawezi kuzungumzia sakata lake na kwamba akili yake ipo kufikiria mchezo wa kesho dhidi ya timu hiyo.

Yanga inashuka ugenini leo kupambana dhidi ya Azam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

“Siwezi kuzungumzia hilo la Feisal ingawa ilitushtua lakini kwasasa tunatakiwa kuangalia jukumu letu zito lililopo mbele yetu, akili yetu sasa ni mchezo wa kesho dhidi ya Azam,” amesema Nabi.

“Tunahitaji ushindi kesho bado tupo kama familia, tunajipanga na hii mechi kubwa, ngumu na muhimu, naamini hata viongozi wetu wanachama na mashabiki wanafikiria tunashindaje vizuri kesho.”

Yanga ambao ni vinara wa ligi wanakutana na Azam kesho katika mchezo wa pili msimu huu baada ya mechi ya awali mabingwa hao watetezi wa ligi kulazimisha sare ya mabao 2-2 huku mabao yao yakifungwa na Feisal ambaye huenda kesho akaukosa mchezo huo.

SOMA NA HII  ULE MZIGO WA PAZIA UNAENDELEA KURINDIMA MUBASHARA NDANI YA DStv.....CHAKUFANYA NI KUSELELEKA NAO VILE VILE...