Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA KUWAVAA WAARABU LEO….JEURI YA YANGA LEO IKO HAPA...

SAA CHACHE KABLA YA KUWAVAA WAARABU LEO….JEURI YA YANGA LEO IKO HAPA ….

Habari za Yanga

ZIKIWA zimesalia saa chache kabla ya Mabingwa wa Tanzania Yanga kushuka Uwanja wa ugenini dhidi ya CR Belouizdad kuna mechi sita zitakazowapa presha Waarabu hao.

Yanga itashuka Uwanja wa 5 Julliet 1962 jijini Algers, Algeria saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kupambana na Belouizdad katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakati Yanga ikiwa na hesabu za mchezo huo kuna matokeo sita ambayo yatawafanya Waarabu hao kuwa makini mbele ya Mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania.

Mechi hizo sita, Yanga imezicheza msimu uliopita ikishinda kwenye viwanja vigumu katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ikianzia hatua ya mtoano Yanga ilitinga makundi ya Kombe la Shirikisho kwa kuwatupa nje Club Africain ya Tunisia ikiwachapa nyumbani bao 1-0, wakitangulia kulazimishwa suluhu nyumbani.

Yanga ilipotinga makundi ilishinda mechi moja ugenini dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo bao 1-0 ukiwa ni ushindi pekee wa ugenini kwao kwenye mechi zao tatu ambapo nyingine ikitoa sare na kupoteza moja na kuongoza kundi lao.

Hatua ya Robo Fainali, Yanga ilianza kwa ushindi ugenini mbele ya Rivers United ya Nigeria mabao 2-0 na kuwatupa nje wapinzani wao hao.

Nusu Fainali ya mashindano hayo walikutana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambapo baada ya ushindi wa mabao 2-0 nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga ilijihakikishia tiketi ya kucheza Fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 ugenini mbele ya ‘Wasauz’ hao.

Ikicheza Fainali yao ya kwanza ya kihistoria Yanga baada ya kuanza vibaya kwa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya USM Alger, walipindua meza na kuwachapa Waarabu hao kwao kwa bao 1-0 kwenye Uwanja huo huo wa 5 Julliet 1962.

Yanga walilikosa taji hilo kwa faida ya bao la ugenini iliyowanufaisha Waarabu hao ambapo leo watarudi kwenye Uwanja huo huo wa 5 Julliet 1962 walipoishia kwenye Shirikisho kumenyana na Belouizdad.

SOMA NA HII  KUELKEA DIRISHA DOGO....FEI TOTO ATAJWA RASMI SIMBA...ISHU NZIMA IKO HIVI...