Home Simba SC KOCHA AS VITA : SIMBA WALIKUWA BORA KWENYE MBINU

KOCHA AS VITA : SIMBA WALIKUWA BORA KWENYE MBINU


BAADA ya kuchezea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Simba kocha mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge ameukubali mziki wa Simba kwa kusema kuwa wapinzani wao hao walikuwa bora zaidi katika mbinu.

AS Vita ikiwa nyumbani katika uwanja wa, Des Martrys de la Pentecote walipoteza dhidi ya Simba kwa kufungwa bao 1-0 lililofungwa kwa njia ya penati na mshambuliaji wa Simba Chris Mugalu.

Akizungumzia ubora wa Simba katika mchezo huo, kocha Ibenge amesema kuwa timu yake haikuwa bora.

“Timu yangu haikuwa bora dhidi ya wapinzani wetu, Simba walifahamu namna gani ya kucheza na sisi wakiwa ugenini, hivyo ubora wa wachezaji wangu ulikuwa chini katika kupangua mbinu za Simba.

“Nawapongeza wapinzani wetu kwa hilo lakini bado kuna safari ndefu japo si njema kupoteza tukiwa nyumbani, tunahitaji kuboresha ili tujiweke katika nafasi nzuri katika kundi letu,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO NA AL AHLY...CEO SIMBA AWEKA SILAHA HIZI HADHARANI...