Home Habari za michezo BAADA YA ‘KUTUSULIWA’ NA YANGA JANA….ZORAN MAKI AKITAZAMA KIKOSI CHAKE WEE…KISHA AKAGUNA...

BAADA YA ‘KUTUSULIWA’ NA YANGA JANA….ZORAN MAKI AKITAZAMA KIKOSI CHAKE WEE…KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HAYA…


Zoran Maki, Kocha Mkuu wa Simba, amesema kuwa, msimu huu wa 2022/23, hautakuwa mwepesi kwa sababu kila timu inahitaji kufanya vizuri.

Maki ana kibarua cha kurejesha mataji ndani ya Simba baada ya msimu wa 2021/22 timu hiyo kuyeyusha yote matatu ambayo ni Ngao ya Jamii, Kombe la Shirikisho la Azam Sports na Ligi Kuu Bara.

 Maki alisema wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya na wanatambua kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya.

“Wachezaji wanatambua kwamba watakuwa na msimu ambao una ushindani mkubwa, hivyo kuna kazi kubwa ya kufanya kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu.

“Ambacho ninafurahi ni kuona kwamba yale ambayo tunafundishana wanaelewa na kuyafanyia kazi, hivyo tutapambana katika kuhakikisha tunacheza mpira mzuri na kupata ushindi,” alisema Maki.

SOMA NA HII  BODI YA LIGI YAILAMU YANGA KWENYE DABI YA KARIAKOO, KISA HIKI HAPA