Home Habari za michezo HAYA HAPA MATOKEO YA LEO LA LIGI KUU YA NBC….YANGA ‘WAHEMEWA’…NTIBAZONKIZA ‘AMCHOKONOA’...

HAYA HAPA MATOKEO YA LEO LA LIGI KUU YA NBC….YANGA ‘WAHEMEWA’…NTIBAZONKIZA ‘AMCHOKONOA’ MAYELE…

Habari za micehzo leo

MBEYA City wamekubali kugawana pointi mojamoja na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Sokoine.

Ni Mbeya City walitangulia kufunga mabao mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa George Sangija dakika ya pili na lile la pili likifungwa na Richardson Ng’odya aliyefunga mabao mawili.

Bao la pili alifunga dakika 53 ikiwa ni kipindi cha pili na Yanga waliweka usawa kupitia kwa Bernard Morrison dakika ya 64 kwa mkwaju wa penalti.

Habari za Michezo leoSure Boy alipachika bao la pili dakika ya 68 wakati Mbeya City wakisubiri mpira uishe Morrison aliwatungua bao dakika ya 90.

Wachezaji wawili wameonyeshwa kadi nyekundu Hassan Nassoro wa Mbeya City na Jesus Moloko wa Yanga dakika ya 87.

Aidha katika mechi nyingi hii leo, IDRIS Mbombo nyota wa Azam FC amefikisha bao lake la 8 Uwanja wa Mkwakwani wakisepa na pointi tatu dhidi ya Coastal Union.

Habari za Michezo leo

Katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo ubao umesoma Coastal Union 0-2 Azam FC.

Mbombo alitupia kambani bao la kuongoza dakika ya 58 ambalo liliwaongezea nguvu Azam FC.

Kwenye mchezo huo dakika 45 za mwanzo zilikamilika bila timu hizo kufungana.

Ni Prince Dube wa Azam FC alipachika bao dakika ya 90 likiwa ni bao la ushindi kwa Azam FC.

Katika mechi nyingine iliyochezwa Chamazi Complex hii leo, Kikosi cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa mzunguko wa pili, Uwanja wa Azam Complex.

Mzawa Israel MwendaΒ amepachika bao moja kwenye mchezo wa leo dakika ya 65 akitumia majalo ya Shomari Kapombe.

Habari za Michezo LeoMabao matano kwa Simba yamefungwa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 15,20, 26, 78 na dakika ya 89.

Anafikisha mabao 15 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 akiwa ni namba mbili kwa utupiaji na namba moja ni Fiston Mayele mwenye mabao 16 kibindoni ni mali ya Yanga.

Bao la kufutia machozi kwa Polisi Tanzania ambayo haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi limefungwa na Henck Mayala dakika ya 85 akimtunga Ally Salim

SOMA NA HII  ENDORPHINE FAIRYTALE -SHANGWE LA SLOTI DISEMBA HII! CHEZA NA UJISHINDIE ZAWADI KABAMBE ZA FEDHA...!