Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Ally Said amesema kuwa hajawahi kuwa na tatizo lolote lile na kiungo wa klabu hiyo, Feisal Salum.
Eng. Hersi anasema Walijaribu Kulizungumza Swala la Feisal Personal (Nje Ya Taasisi) ili kuangalia namna gani wanalimaliza, ikiwemo na baadhi Ya Viongozi Kuingilia kati Lakini Msimamo wa Feisal ulibaki palepale kwamba hataki kurudi Yanga Sc .
Hivyo Basi kwa sasa kilichobaki ni kufuatwa kwa misingi ya Klabu na Sheria na sio huruma tena.
Eng Hersi amesema kwamba yeye ni Rais wa Klabu hivyo ni Lazima asimamie Interest (Matakwa) ya klabu na sio kuingiza huruma kwenye suala hili.
Maneno hayo yalisemwa na Injinia Hersi kabla ya Rais Samia Kutoa ombi lake kwa klabu ya Yanga kutaka walimalize jambo hilo.
Jana Rais Samia Suluh Hassan aliwataka Yanga kumalizana na Fei Toto huku akisema kuwa si vyema klabu kubwa kama hiyo kuzozana na ‘katoto’
Dr Samia alisema hayo kwenye dhifa ya kitaifa aliyowanadalia wachezaji na viongozi wa Yanga ikiwa ni siku chache baada ya kufanikiwa kumaliza wa pili kwenye shindano la kombe la shirikisho Afrika, ambapo walicheza na USMA ya Algeria.
Sakata la Fei toto na Yanga limechukua sura mpya hivi karibuni, mara baada ya kiungo huyo mzanzibari kuibuka hadharani kwa mara ya kwanza kwenye chombo cha habari kuzungumza kiundani kuhusu jambo hilo.
Katika mahojiano yake na Clouds Media mapema wiki iliyopita. Fei Toto alisema kuwa yuko tayari kurudi Yanga endapo Injinia Hersi atajiuzulu Uongozi ndani ya klabu hiyo ambao pia ni mabingwa wapya wa ligi kuu ya NBC.
SOMA NA HII BAADA YA MAYELE KUPEWA NG'OMBE MOROGORO...SIMBA WAIBUKA NA HILI...WAWEKA MBUZI MEZANI...