Home Habari za michezo WANACHAMA SIMBA WACHARUKA……MANGUNGU,TRY AGAIN WAWEKWA KITIMOTO

WANACHAMA SIMBA WACHARUKA……MANGUNGU,TRY AGAIN WAWEKWA KITIMOTO

Simba SC

Uongozi wa Simba SC, kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi, Salim Abdallah na Mwenyekiti wa Simba SC pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wamekutana na wanachama wa Simba SC ambao walikuwa wanalalamikia Uongozi kwa kumtaka Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu kujiuzulu nafasi yake.

Kwenye Kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Gerezani zimejadiliwa agenda Kuu nne kutoka kwa wanachama ambazo ni Mpasuko ndani ya Klabu, Timu kufanya vibaya, Mabadiliko ya Katiba na Usimamishwaji wa baadhi ya viongozi wa matawi bila utaratibu.

Baada ya kusikiliza Agenda hizo Uongozi wa Simba SC, Kupitia kwa M/Kiti wa Bodi Simba SC, Salim Abdallah na Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu wamekubaliana na wanachama hao Kwanza kuunda Kamati ya maridhiano.

Maridhiano hayo ni pamoja na Uongozi wa Bodi ya Simba SC ukutane na wagombea wote walioshiriki uchaguzi uliopita na kukaa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya Simba SC.

Lakini pia Kikao hicho kimetoa Ushauri wa namna ya kudhibiti kambi kwa maana wanafanya usajili mzuri ila wachezaji huwa hawafanyi vizuri.

Kikao hicho pia kimetazama namna timu yao na baadhi ya wachezaji kuonekana kufanya Hujuma, na wamekubaliana wanalifanyia kazi hilo kwa kuzingatia namna bora ya timu kubaki na balance.

Miongoni mwa makubaliano mengine ni marekebisho ya Katiba na zoezi hilo miongoni mwa wajumbe tarajiwa atakuwepo Advocate Moses Kaluwa ambae alikuwa mgombea wa Uenyekiti Simba SC, na wajumbe wengine watapendekezwa na wanachama waliokuwa wanapinga uongozi watashiriki katika zoezi hilo la kurekebisha katiba ya Simba SC.

Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu amewataka viongozi wote waliosimamishwa bila sababu za msingi warudishwe kwenye nafasi zao

SOMA NA HII  YANGA WAPIGA MOYO KONDE KUHUSU NGAO YA JAMII, WAELEKEZA NGUVU HUKU, UONGOZI WAFUNGUKA