Home news EHEEEH….HUYU KAPOMBE KASHINDIKANA AISEEE…MAMBO ALIYOYAFANYA NI ZAIDI YA ‘CONNECTION’…

EHEEEH….HUYU KAPOMBE KASHINDIKANA AISEEE…MAMBO ALIYOYAFANYA NI ZAIDI YA ‘CONNECTION’…


BEKI wa Simba , Shomary Kapombe kashindikana. Inaweza ikakushangaza, lakini ndivyo ukweli ulivyo kuwa, beki huyo ana rekodi ngumu aliyoiweka karibu misimu sita sasa, enzi akiwa Azam FC na imeshindwa kuvunja hadi leo.

Beki huyo katika msimu wa 2015-2016 akiwa Azam, alifunga mabao nane ambayo yalikuwa mengi kuliko hata baadhi ya washambuliaji wa timu za Simba na Yanga.

Tangu alipofunga mabao hayo kisha kuhamia Msimbazi msimu wa 2017-2018, haijawahi kufikiwa na wala yeye mwenyewe hajaifikia au kuivuka tena kuonyesha rekodi hiyo inaweza kuendelea kuwatesa mabeki nchini kwa muda mrefu.

Kapombe aliwahi kukaririwa akisema, ubora wa Azam kipindi hicho na jinsi alivyokuwa amepewa uhuru na kocha wake, ndio vilivyombeba na kufunga mabao hayo.

Katika msimu uliopita beki wa Biashara United, Lenny Kisu alimaliza akiwa na mabao matano, ambapo yalibakia mabao matatu kufikia idadi ya Kapombe.

Katika ligi inayoendelea kwa sasa beki wa Yanga, Shaban Djuma ana bao moja alifunga dhidi ya Ruvu (penalti), asisti ya mbili alizompa Fiston Mayele dhidi ya Biashara Unite na Coastal Union.

Mabao ya Kapombe

Alifunga bao moja dhidi ya Coastal Union, timu yake ikifunga mabao 2-1, alifunga dhidi Ndanda FC 1-0,dhidi ya Toto Africans mabao mawili, Azam ikishinda mabao 5-0.

Aliifungia dhidi ya Mgambo Shooting mabao 2-0, alifunga dhidi ya Stand United bao 1-0, dhidi ya Kagera Sugar bao moja, Azam FC ikishinda mabao 2-0.

Walifunga ila hawakumfikia

2009/10-JUMA ABDUL-TOTO AFRICA

Ndani ya msimu huo, Juma Abdul akiwa Toto Africans alikuwa wa moto na kuisaidia timu yake kuifungia mabao sita.

2011/12-SAID SWEDI-COASTAL

Said Swedi wakati anaichezea Coastal Union ya Tanga, msimu wa 2011/12 alikuwa kwenye kiwango cha juu na alifunga mabao sita.

2012/13- CANNAVARO, TWITE-YANGA

Mabeki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Mbuyu Twite kila mmoja alifunga mabao manne, hivyo mabeki hao walichangia mabao nane katika msimu wa 2012/13.

2013/14 TUMBA, SWEDI-ASHANTI

Wakati Ashanti inashiriki Ligi Kuu Bara, msimu wa 2013/14 beki Tumba Swedi alimaliza na mabao matano na ndiye beki aliyefanya vyema nyakati hizo.

SOMA NA HII  KWA TAARIFA YAKO...HII HAPA REKODI ALIYOWEKA BOCCO BAADA YA KUFUNGA GOLI MBILI JANA..