Home Azam FC AZAM WAIFANYIA JANJA TFF KUHUSU ISHU YA DABO

AZAM WAIFANYIA JANJA TFF KUHUSU ISHU YA DABO

Kocha Mpya Azam FC

Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limemzuia rasmi Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo, raia wa Senegal kusimama kwenye benchi la ufundi la timu hiyo kutokana na sababu za kutokidhi vigezo ambavyo vinatakiwa.

Dabo ambaye tangu ametua nchini amekuwa akikiongoza kikosi hicho amezuiwa kutokana na Leseni A ya UEFA aliyonayo kutokidhi vigezo vya kanuni za soka la Tanzania ambazo haziruhusu kuwa kocha mkuu wa Ligi Kuu.

Chanzo cha kuaminika kutoka TFF kimeeleza kuwa, Dabo hatambuliki kama kocha mkuu hivyo kutokana na leseni aliyonayo anaruhusiwa kusimamia benchi akiwa kama kocha msaidizi na viongozi wa Azam FC tayari wanalijua hilo.

“Mwanzo alikuwa anakaa na kutambulika kama kocha mkuu kwa sababu awali walisema atakwenda kuongeza elimu yake, lakini baada ya kuona kimya na maneno mengi tukaona tufuate kanuni tulizojiwekea,” kilisema chanzo.

Hata hivyo, inatambulika Mfaransa Bruno Ferry aliyetua ndani ya kikosi hicho akiwa msaidizi wa Dabo ndiye aliyekabidhiwa mikoba ya kuiongoza timu hiyo kutokana na leseni A ya CAF aliyonayo kumruhusu kusimamia benchi.

Hata hivyo, hayo yakiendelea taarifa zinaeleza kuwa licha ya Dabo kutotambulika, wao ndani wanamtambua kama kocha mkuu na ndiye atakayewajibika kwao.

Ferry mwenye umri wa miaka 56 alikuwa kipa nchini Ufaransa huku akiwa na uzoefu mkubwa ambapo amefundisha klabu mbalimbali zikiwemo Eding Sport FC ya Cameroon, Accra Lions ya Ghana na Louhans Cuiseaux ya kwao akiwa kama kocha mkuu.

SOMA NA HII  AKILI YA SIMBA SASA NI KWA COASTAL UNION, MSUTUPANGIE KIPA LANGONI