Home Simba SC RASMI:SIMBA YATAMBULISHA JEMBE LA KAZI

RASMI:SIMBA YATAMBULISHA JEMBE LA KAZI


RASMI kikosi cha Simba leo kimemtambulisha Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal mwenye miaka 24.
Nyota huyo anakuwa ingizo jipya la nne ndani ya Simba baada ya jana Agosti 13 kumtambulisha Duncan Nyoni aliyeungana na Peter Banda pamoja na mzawa Yusuph Mhilu.


Nyota huyo anatajwa kuwa na uwezo mkubwa ndani ya uwanja pale anapopata nafasi akiwa ni kiungo mshambuliaji kinda aliyefanya vizuri kwenye ligi ya Senegal.  

Rekodi zinaonyesha kwamba alitupia mabao 8 na pasi 10 alitoa, pia ndiye mchezaji aliyeng’ara wakati timu ya Teungueth ikiitoa timu ya Raja Casablanca ya Morocco msimu ulioisha na kufuzu hatua ya makundi ya Caf Champions League.

Kwenye kambi nchini Morocco ambapo Simba wapo kwa sasa atajumuishwa na wengine ili kuendelea na maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA KUILIPA SIMBA KWA MAGOLI....MOSES PHIRI AIBUKA NA HILI TENA...AOMBA UTAMBULISHO MPYA...