Home Habari za michezo KIONGOZI WA YANGA AFUNGUKA KUHUSU KUMFUKUZA ROBERTINHO

KIONGOZI WA YANGA AFUNGUKA KUHUSU KUMFUKUZA ROBERTINHO

Habari za Simba SC

Makamu Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kama angekuwa kiongozi wa Simba SC basi tayari angekuwa amemtimu kocha wa Simba Robertinho kwasababu ni mchekeshaji (Comedy).

Akizungumza kupitia bongo5 Mwakalebela amekiri kuwa Simba SC ipo vizuri na ina wachezaji wazuri lakini tatizo la Wekundu hao wa Msimbazi ni benchi la ufundi (technical bench)

Mwakalebela amegusia suala la Mwamuzi akidai haelewi “kama wanakulaga (Simba) mayai na waamuzi sijui lakini kuna fairness fulani wanakosa. Marefarii sijui wana tatizo gani, nashindwa kuelewa kwanini kwenye mechi za Simba tu”

Aidha Makamu Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga amesema haoni nafasi ya Simba kufika nusu fainali wala robo ya CAF Champions League kama Aish Manula hatokaa golini.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO YANGA NA RAIS SAMIA WALIVYOAMSHWA SHANGWE LA 'KUFA MTU' JANA MALAWI...