Home Habari za michezo MARAIS HAWA KUISHUHUDIA SIMBA VS AL AHLY

MARAIS HAWA KUISHUHUDIA SIMBA VS AL AHLY

Tetesi za Usajili Simba

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula, amesema marais wa FIFA na CAF ni miongoni mwa watu mashuhuru watakaofika kushuhudia mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Al Ahly na Misri.

Simba wanatarajia kushuka dimbani kwenye mchezo huo wa uznduzi wa michuano ya Africa Football League Oktoba 20 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

“Tunaishukuru serikali kwa matengezo makubwa ambayo imefanya kwenye Uwanja wa Mkapa. Simba pia imetoa mchango kiasi kufanikisha hili.”

“Rais wa FIFA atakuwepo, Rais wa CAF atakuwepo na marais wa vyama vya soka vya maeneo mengine hivyo inahusisha vyombo vingi za serikali.”

“Tunajua kutakuwa na watu mbalimbali kutoka mikoani na jana tulikuwa na mkutano na @AirTanzania ili kupata punguzo la bei ya tiketi kwa mashabiki wa Simba kutoka mikoani.”

“Lengo letu ni uwanja kujaa watu 60,000. Tunatarajia tiketi zitauzwa kwa haraka hivyo tiketi zikitangazwa watu wanunue kwa haraka sababu tunatarajia watu wengi kutoka nje ya Dar. Tiketi za makundi zitaendelea kuwepo (Mnyama Package).”

“Kesho kuna jambo, tuliache liwe maalumu kuelekea mchezo wa African Football League na kutakuwa na matukio kila siku hadi siku ya mchezo,” Lisema CEO Imani Kajula.

SOMA NA HII  MAYELE AFUNGUKA ALICHOMSHAURI FEI TOTO KABLA YA SAKATA LAKE