Home news SERENGETI BOYS WAPAA KWENDA MOROCCO KWENYE MICHUANO YA AFCON U-17

SERENGETI BOYS WAPAA KWENDA MOROCCO KWENYE MICHUANO YA AFCON U-17


MCHANA wa leo timu ya taifa ya soka kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imesafiri kwenda nchini Morocco kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana wasiozidi umri huo (Afcon U-17).

Kikosi hicho kimesafiri na jumla ya wachezaji 22 ambao wataambatana na benchi la ufundi la timu hiyo na vingozi wengine wachache walioteuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti kabla ya kuanza safari kocha mkuu wa timu hiyo Hababuu Ali amesema wanaenda kupambana na kuhakikisha wanailetea heshima nchi.

“Tupo vizuri na vijana tumewaambia tunachohitaji hivyo tuanenda kupambana kwa maslahi makubwa ya nchi ili tukirejea tuwe na heshima kubwa,” amesema Hababuu.

Wachezaji Shomari Mbwana Mnyaman , Said Naushad Said, Liptone Eliabi Mlugulwa, AbdulKarim Kassim Kiswanya, Abubakar Abdallah Sabiani, Omary Hassan Yahya, Abdurhaman Juma Kerry, Mohamed Saad Hussein, Kelvin Joel Komba, Omar Abas Mvungi, Omary Bakari Omary, Abdallah Hamis Hassan, Sylvester Sylvester Otto, Ahmed Kharid Chambera, Baraka Sylvester Nyamkindo, Kassim Ibrahim Yahya, Ismail Mpank Bombama, Hijjah Shamte Lidah, Ladaki Juma Chasambi, Kamli Jesto Masanja, Abdallah Mussa Libandika na Abubakar Ramadhan Lubotile ndio watakaoiwakirisha nchi katika michuano hiyo.

Hii ni kwa mara ya tatu kwa Serengeti Boys kushiriki michuano hiyo ambapo kwa mara ya kwanza ilikua mwaka 2017 ikifanyika Gabon na mara ya pili ilikua 2019 ilipofanyika hapa Tanzania na mara zote hizo timu hiyo imekuwa ikiishia hatua ya makundi.

Katika michuano ya mwaka huu, Serengeti Boys imepangwa Kundi B pamoja na timu za Nigeria, Algeria na Congo huku mechi yao ya kwanza wakitarajia kucheza Machi 14 mwaka huu dhidi ya Nigeria.

SOMA NA HII  MANARA:..KUNA ZAMBI INATENGEZWA KUHUSU MWAMNYETO...HATUWEZI KUISHI KWA KUKARIRI...