Home Habari za Yanga HIVI NDIVYO YANGA NA RAIS SAMIA WALIVYOAMSHWA SHANGWE LA ‘KUFA MTU’ JANA...

HIVI NDIVYO YANGA NA RAIS SAMIA WALIVYOAMSHWA SHANGWE LA ‘KUFA MTU’ JANA MALAWI…

Habari za Yanga leo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Dk Lazarus McCarthy Chakwera, wamekutana na kikosi cha Yanga kilichowasili Julai 5, 2023 nchini Malawi kwa mualiko maalumu wa Rais wa nchi hiyo.

Rais Samia amekutana na timu hiyo wakati akiwasili nchini Malawi ambapo amehudhuria sherehe za miaka 59 ya uhuru wa taifa hilo zitakazofanyika Julai 6, 2023.

Kikosi cha Yanga kimeshiriki katika mapokezi ya Rais Samia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu Lilongwe nchini Malawi.

Yanga wapo nchini humo ambapo watashiriki sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa taifa hilo kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Nyasa Big Bullets ya nchini humo.

SOMA NA HII  GAMONDI AWAFANYIA UMAFIA MASHABIKI WA YANGA, ISHU IKO HIVI