Home Habari za michezo ACHANA NA MASTAA WAPYA….MAKOCHA WAPYA WATAKAO MSAIDIA MBRAZILI SIMBA HAWA HAPA..

ACHANA NA MASTAA WAPYA….MAKOCHA WAPYA WATAKAO MSAIDIA MBRAZILI SIMBA HAWA HAPA..

Tetesi za Usajili Simba

KATIKA kuhakikisha wanaimarisha benchi la ufundi la Simba, tayari viongozi wa klabu hiyi uko kwenye mazungumzo ya mwisho na aliyekuwa mtaalamu wa mazoezi ya viungo wa Vipers FC ya Uganda, Raia wa Rwanda Hategekimana Corneolle.

Corneolle anakuja kuchukuwa nafasi ya Kelvin Mandla aliyekuwa katika nafasi hiyo kwa msimj uliomaliza hivi karibuni kwa kusitishiwa mkataba wake ndani ya klabu hiyo.

Chanzo makini kilichoifikia jana, kuwa Kocha huyo sa Viungo raia wa Rwanda yupo nchini baada ya kuwasili jana usiku wa manane na muda wowote watamtambulisha.

Chanzo hicho kilisema tayari kocha huyo ametua nchini baada ya mapendekezo ya mwalimu Mkuu Roberto Oliveira (Robertinho) aliyetua jana Alfajiri kwa ajili ya kuanza maandalizi rasmi.

“Tayari kocha wetu wa viungo ameshatu nchini n muda wowote tutamtumbulisha baada ya kukamilisha mipango yote ya kimakataba,” alisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema mambo mazuri yanakuja na kuhusu makocha wa viungo, kipa watatangazwa muda wowote.

Alisema rasmi wataanza kutambulisha vifaa vyao vipya lakini wanaanza na benchi la ufundi kwa nafasi tatu zilizoachwa wazi ikiwemo kocha wa viungo, makipa na daktari.

“Mashabiki wasiwe na presha yeyote uongozi upo makini kuanzia kuimarisha benchi la ufundi kwa zile nafasi tatu za wazi na tutawatangaza muda wowote, baada ya hapo tutawatambulisha wachezaji wapya,” alisema Ahmed.

Aliongeza kuwa mara baada ya utambulisho huo benchi hilo jipya likiongozwa na Roberto Oliviera (Robertinho) wataungana na wachezaji wapya kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kambi.

Simba wanatarajia kuondoka nchini Julai 11, mwaka huu na watakaa huko kwa muda wa wiki tatu na wanatarajia kucheza mechi tatu za kirafiki ya kimataifa kujiandaa na msimu 2023/24 wa Ligi Kuu, michuano ya kimataifa na Super League.

SOMA NA HII  AISEEE!! HII SASA KUFURU...JINA LA PELE LAWEKWA KWENYE KAMUSI