Home Habari za michezo PAMOJA KUZIBULIWA JUZI NA VIPERS ….STAA ALIYEKIPIGA EPL AIBUKA NA HILI...

PAMOJA KUZIBULIWA JUZI NA VIPERS ….STAA ALIYEKIPIGA EPL AIBUKA NA HILI KUHUSU YANGA YAKE NA MECHI YA SIMBA…


Kiungo wa Yanga, Gael Bigirimana, ameanza na mkwara mzito kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba kwa kuwaambia wapinzani wao kwamba, wanapaswa kujipanga vizuri na wasipumbazwe na kipigo walichokipata toka kwa Vipers wikiendi iliyopita.

Bigirimana aliyewahi kucheza Ligi Kuu ya England akiwa na Newcastle United, amejiunga na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Glentoran ya Ireland Kaskazini.

Bigirimana amesema kuwa;

“Binafsi kwangu utakuwa ni mchezo muhimu kwa sababu ni dabi ambayo imekuwa ikifuatiliwa na watu wengi Afrika Mashariki na Kati.

“Kwa upande wangu nitakachokiangalia ni suala moja la kuhakikisha nakuwa msaada wa timu kupata ushindi.

“Simba ni moja kati ya timu kubwa kama ilivyo Yanga, lakini jambo la msingi kwetu ni kuwaheshimu kama watani, lakini suala la kupata matokeo ni kipaumbele chetu cha kwanza kwa kuhakikisha rekodi ya msimu uliopita tunaiendeleza.”

Yanga ilipoteza kwa mara ya kwanza Jumamosi iliyopita mchezo wa kirafiki dhidi ya Vipers SC ya Uganda kwatika maadhimisho ya Kilele cha “Siku ya Mwananchi”

SOMA NA HII  WAKATI MAKAMBO AKIANZA KUTUPIA YANGA...MAYELE APATA 'PANCHA'..AINGIA UWANJANI AKICHECHEMEA...