Home Burudani BAADA YA KAONEKA KULALAMIKA MANDONGA ANAPEWA UMAARUFU NA MADILI…MANDONGA AIBUKA NA KUMJIBU...

BAADA YA KAONEKA KULALAMIKA MANDONGA ANAPEWA UMAARUFU NA MADILI…MANDONGA AIBUKA NA KUMJIBU KWA STAILI HII…


Mabondia Karim Mandonga na Shaban Kaoneka wamerudi tena kwenye headlines kufuatia kauli ya Kaoneka aliyoitoa wakati akihojiwa na vyombo vya habari kwenye Tamasha la Simba Day katika Dimba la Mkapa.

Kwenye mahojiano hayo Kaoneka alisema, “Mandonga amepata bahati kuliko mimi, waandishi wa habari wakati mwingine naona kama mnakuwa wanafiki, hamjaniita hata ofisini kwenu kunihoji, mbona Mandonga mnamfanyia surprise nyingi, mimi niliyeshinda nakuwa masikini, aliyepigwa anakuwa tajiri,” alieleza Shabani Kaoneka akiiambia Wasafi Media.

Kauli hiyo imemuibua Karim Mandonga Mtu Kazi ambaye hivi karibuni amelamba madili mbalimbali, yeye ameeleza kuwa, hata yeye hajawahi kuwaza kama kuna siku atasimama kama mtu maarufu mkubwa hivyo Kaoneka hapaswi kumlaumu mtu yoyote yule. Ajifunze kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

“Dah Shabani ndugu yangu me naamini kabisa ridhiki inatoka kwa mafungu na kwa muda maalumu alieupanga Mungu suala la nani afanikiwe nani aishie njiani ni majukumu ya Allah mimi na wewe hatupaswi kumlaumu mtu yoyote yule.

“Katika tasnia hii ya mchezo wa ngumi na watu wa media kiujumla hata mimi sijawahi kuwaza kwamba ipo siku nitasimama kama SUPERSTAR MKUBWA but all in all tujfunze kumshukuru Mungu kwa kila jambo. KAMA IPO IPO TU” ameandika Bondia Karim Mandonga.

SOMA NA HII  FEI TOTO AWAPA NENO YANGA WATAJUA HAWAJUI