Home Uncategorized HOFU YA NAMUNGO IPO HAPA

HOFU YA NAMUNGO IPO HAPA


UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa kwa sasa hesabu zao kubwa ni kuona kwamba timu yao inapata nafasi ya kuleta ushindani wa kweli hivyo kazi yao ya kwanza itakuwa ni kujilinda kutokushuka Daraja.

Akizungumza na Salehe Jembe, Kocha Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery amesema kuwa kwa sasa malengo makubwa ya timu ni kucheza soka la kweli litakalowasaidia kutokushuka Daraja.

“Hatari kubwa kwa timu ngeni kwenye ligi ni kushuka daraja, malengo yetu ya kwanza ni kuona tunacheza soka safi, kisha mengine yatafuata.

“Kwa kuligundua hilo tumeanza na mkakati wa kusajili wachezaji makini na wenye uzoefu na nina imani watatusaidia,” amesema.

Namungo FC ni timu yenye maskani yake Lindi, ni miongoni mwa timu 20 ambazo zitashiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

SOMA NA HII  NDINGA MPYA KABISA KWA MIA NANE TU AMA JERO, NI RAHISI FANYA HIVI