Home Namungo FC NAMUNGO FC YAREJEA BONGO, TAYARI KWA LIGI KUU BARA

NAMUNGO FC YAREJEA BONGO, TAYARI KWA LIGI KUU BARA


 KIKOSI cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Moroco leo Aprili 12 kimerejea Tanzania kikitokea nchini Zambia ili kuendelea na mechi zake za Ligi Kuu Bara.

Namungo jana Aprili ilikuwa na kibarua cha kuipeperusha Tanzania kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Nkana FC.

Mchezo huo dakika 90 zilikamilika kwa Nkana FC kushinda bao 1-0 dhidi ya Namungo na kufanya kikosi hicho kilicho kwenye kundi D  kupoteza mechi zake mbili mbele ya Nkana FC.

Ule wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Namungo 0-2 Nkana FC. Kwenye kundi D Namungo FC ipo nafasi ya nne bado haijakusanya pointi.

Morocco amesema:”Tumeshawasili tayari Tanzania muda huu, tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumerejea salama,” . 

SOMA NA HII  LUSAJO: - MSINISHINDANISHE NA MAYELE...MNANIPA PRESHA...,UNAWEZA UKAPATA MAJERAHA...