Home Uncategorized AZAM FC WAZIDI KUJIFUA, WATUMA UJUMBE HUU KWA WAPINZANI WAO

AZAM FC WAZIDI KUJIFUA, WATUMA UJUMBE HUU KWA WAPINZANI WAO


JAFFARY Maganga, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kikosi kinaendelea na maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kesho, Januari 27 dhidi ya Friend Rangers utakochezwa Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo ni wa hatua ya 32 bora ya kombe hilo ambalo lipo mkononi mwa Azam FC.

“Kikosi kipo salama na maandalizi yapo vizuri, utakuwa mchezo mzuri na mgumu mashabiki wajitokeze kutupa sapoti,” amesema.

Taji la Shirikisho, Azam FC walilitwaa kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Lipuli FC na bao la ushindi lilifungwa na Obrey Chirwa.

SOMA NA HII  MZEE MAGALI ALIVYOMWEKEA UPUPU MWALIMU WAKE